Imekuwa
kama ambavyo wengi walitabiri kutokana na mafanikio aliyopata akiwa na timu
yake ya taifa pamoja na klabu, Mohamed Salah wa Misri ameshinda tuzo ya
mchezaji bora wa Afrika mwaka 2017 akiwashinda wenzake Sadio Mane aliyeibuka
mshindi wa pili na Pierre Emerick Aubameyang aliyeshinda nafasi ya tatu.
Mwaka
2017, Salah amejipambanua baada ya kuisaidia Liverpool aliyojiunga nayo
akitokea AS Roma ya Italia, kwa kuifungia magoli 23 katika mechi 29 alizocheza,
lakini zaidi akiisaidia timu yake ya taifa ya Misri kuweka historia iliyofutika
miaka 25 iliyopita ya kufuzu kombe la dunia.
Hii
ni kubwa ya tatu ya kimataifa ya nyota huyo katika baada ya kunyakua tuzo ya
mchezaji bora kutoka mataifa ya kiarabu, mchezaji bora wa Afrika wa Tuzo za
BBC.
Katika
tuzo za jana zilizofanyika mjini Accra nchini Ghana, Mwanadada Asisat Oshola
alishinda tu Soka, Uingereza:zo ya mchezaji bora kwa wanawake na mchezaji bora
chipukizi akiibuka Patson Daka kutoka Zambia.
Timu
ya taifa ya Misri ilitangazwa kuwa timu bora ya mwaka kwa wanaume na timu ya
wanawake ya Afrika Kusini ikitangazwa timu bora ya mwaka 2017.
Wydad
Casablanca ya Morocco ndiyo klabu bora ya soka ya mwaka na kocha Hector Cuper
wa timu ya taifa ya Misri akitangazwa kocha bora wa mwaka 2017.
Lakini
tuzo za heshima kwa viongozi na watu mashuhuri, Mzee Ibrahim Sunday ambaye
alikuwa mchezaji maarufu kutoka Ghana katika miaka ya 66, Nyingine ilikwenda
kwa Ahmed Yahya wa Mauritania aliyetangazwa kiongozi bora wa soka.
Wengine
waliopewa tuzo ya heshima ya juu ni Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo ambaye
alihudhuria hafla hiyo ya utoaji tuzo, pamoja na George Weah ambaye ni
mwanasoka wa zamani na Rais Mpya wa Liberia.
0 comments:
Post a Comment