MKUU wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge aitaka Manispaa Dodoma na SIDO) kuanisha wenye viwanda vidongo ili watengewe maeneo



MKUU wa mkoa wa Dodoma  Dk Binilith Mahenge ametoa mwezi moja kwa uongozi wa manispaa, Shirika la viwanda vidogovidogo  ( SIDO) na   kuhakikisha wanaanisha maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara wa viwanda vidogovidogo.
Dk Mahenge ameyasema hayo jana wakati wa ziara yake ya kikazi alipotembelea viwanda vidogo vidogo vilivyopo mkoa Dodoma.

Amesema kila kundi wakiwemo wafanyabiashara wa kusaga na kukoboa mchele, wenye viwanda vya  kukamuwa mafuta ya alzeti, mamalishe na  fundi selemala  utasaidia kujua idadi yao  na kuweza kuajiri watu wengi kwa muda mwafaka.
Aidha amesema kama watatengewa maeneo yao na kuwekwa pamoja kutasaidia kupata huduma kiurahisi ikiwemo huduma za umeme,kupata mikopo kiurahisi, kuwasaidia wapeleka bidhaa kama alzeti na wahitaji kufikiwa kwa haraka pia hata kufikiwa na serikali
Mbali na hayo Dk Mahenge  amesema   lengo la ziara yake ni kuwatambua wafanyabiashara hao na kujua changamoto wanazokumbana nao kama wajasiliamali.
Awali akizungumza Kaimu meneja wa SIDO Stephano Ndugulu amesema wao kama Sido kazi yao ni kuzalisha mashine kwa ajili ya wajasiriamali zikiwemo za kusaga na kukoboa na kudai kuwa mafunzo yatolewayo ni pamoja na mafunzo ya kujitambua,mafunzo ya usimaminzi wa biashara na mafunzo ya kiufundi.
Hata hivyo amesema  huduma zitolewazo  na shirika hilo  ni  pamoja na Masoko na uwekezaji ili kupata maeneo ya kuwekeza lengo ikiwa ni kujenga mtandao wa biashara  na kuweza kutambua jinsia yamtu mwingine anavyofanya.
Kwa upande wake Mmiliki  wa kiwanda  ukamuaji wa mafuata ya alizeti kiitwacho  Jackma kilichopo Kikuyu mjini hapa amesema changamoto kubwa wanaipata kama wafanyabiasaha ni pamoja na eneo la uwekezaji ni dogo ambapo hupeleka kushindwa kutanua  biashara yao.
Licha ya hayo ameongeza kuwa kiwanda chache kwa siku kinakamuna  mafuta tani saba awali kilikuwa kinakamua  gunia kumi hii ni kutokana na kuongeza idadi za mashine zenye thamani ya shilingi  milioni 290 kwa kila mashine ya uzalishaji na kudai kuwa mpaka sasa ameajiri wafanyakazi 15 na watu 2450 ndio wanaopeleka alizeti katika kiwanda chake.
Naye mmiliki wa kiwanda cha kusaga na kukoboa Mchele Kiitwacho  kato kilichopo majengo sokoni mjini Dodoma Ernest Kato amesema anaiomba serikali  kuwamilikisha maeneo ili waweze kujenga makazi ya kudumu kwa kuwa wao kama wawekezaji wako tayari kupatiwa maeneo mengine.
Katika ziara yake Mkuu wa mkoa ametembelea viwanda mbalimbali kikiwemo kiwanda cha asante kilichokuwa kinatengeneza maji ya Asante kilichopo Ntyuka,  Mamalishe waliopo majengo sokoni, ‘ Advema Leather Product’ Kilichopo Mailimbili ,Kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti Jackma,kiwanda cha kusaga na kukoa Mchele Kato kilichopo Majengo pia ameweza kutembelea mafundi Selemala wa  Bairodi na kipande mjini hapa.



Share on Google Plus

About NYEMO FM RADIO

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment