Msanii filamu na video vixen, Suzan
Michael maarufu kama Pretty Kind amefunguka na kuomba radhi kwa Serikali na
Watanzania kwa ujumla kutokana na vitendo vyake vya kupiga na kuweka picha
mitandaoni za nusu uchi.
Akiongea
jana na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufungiwa na serikali
kujihusisha kufanya kazi zozote za sanaa kwa miezi sita, Pretty Kind alisema
kuwa amejifunza na kugundua kuwa alikuwa anafanya makosa hivyo sasa hataweza
kurudi tena kufanya mambo hayo.
“Naomba
niombe radhi kwa Watanzania wote kwa hiki nilichokifanya natambua nimefanya
kosa naomba msamaha aweze kunisamehe, pia naomba msamaha kwa mashabiki zangu
kwa hiki kilichotokea nimejifunza hivyo nitakuwa Pretty Kind mwingine mpya na
kufanya yale yanayotakiwa katika jamii” alisema
Pretty
Kind amefungiwa kujihusisha na sanaa kwa takribani miezi sita baada ya kuposti
picha katika mtandao wake wa Instagram ikimuonyesha akiwa nusu utupu jambo
ambalo ni kinyume na maadili ya Kitanzania na kwenda kinyume na maagizo ya Rais
John Pombe Magufuli ambayo aliyatoa hivi karibuni kuwataka wasanii wa kike
kuvaa kwa staha.
0 comments:
Post a Comment