Rais Dkt. John Pombe Magufuli
amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam
(UDSM) kuwa Kamishna wa Madini.
Rais ametangaza
uteuzi huo leo Jumatatu Januari 8, 2018 alipokuwa akitoa hotuba fupi mara baada
ya kumuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini.
“Nimesikia
tatizo ni kamishna wa madini, sasa nimeamua kumteua kamishna mpya wa madini,
jina lake linaanza na Prof. Shukrani Elisha, huyo atakuwa ndiye mtendaji na
msimamizi mkuu wa madini.
“Mambo ya
hovyo ni mengi mno, nilipotembelea bandarini niliunda katume kasirisiri hivi,
kwa kulihusisha Jeshi la Wananchi, TISS na Polisi. Yanayogundulika huko ni ya
ajabu, kuna hadi simenti za zamani sana, yapo makontena bandarini na pale
Ubungo.
“Mimi sio
mwanasiasa mzuri wa kubembelezabembeleza, nikitoka mimi mtapata wakubembeleza,
ila mimi nataka kabla ya Ijumaa regulations (kanuni za sheria ya madini) ziwe
zimesainiwa. Pro Kabudi nendeni mkazifanyie kazi, tafuta watu wa kukusaidia na
mkamalize hayo,” alisema Magufuli.
Kamishna
aliyekuwepo, Mhandisi Benjamin Mchwampaka amehudumu katika nafasi hiyo
kwa siku 263 tangu alipoteuliwa mpaka leo uteuzi wake ulipotenguliwa na Rais
magufuli.
Aidha rais Magufuli amewataka watendaji wote wa Wizara ya Madini kuchapa kazi kwa bidii kwani mpaka sasa bado utendaji wao bado unasuasua.
Aidha rais Magufuli amewataka watendaji wote wa Wizara ya Madini kuchapa kazi kwa bidii kwani mpaka sasa bado utendaji wao bado unasuasua.
0 comments:
Post a Comment