Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai
amempa pongezi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
kwa kuweza kusikiliza maoni ya Bunge na wabunge kwa kutekeleza moja ya maombi
yao kuigawa Wizara ya Nishati na Madini.
Ndugai
ametoa pongezi hizo leo Januari 8, 2018 akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam katika
hafla ya kuapishwa kwa Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Mashaka Biteko na
kusema kwa miaka mingi walikuwa wakitaka Wizara hizo kugawanywa lakini ilikuwa
inashindikana ila katika awamu ya tano Rais Magufuli ndiyo ameweza kufanya
hivyo.
"Sisi
Bunge tulikuwa tukishauri toka miaka ya nyuma kwa Serikali kwamba Wizara
iliyokuwa inaitwa Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa ni nzito mno, ilikuwa
imejaza mambo mengi sana kwa wakati mmoja ushauri wetu ulikuwa ni vizuri
kuzitenganisha na kuzisimika kila moja kivyake.
"Jambo
hili Mhe. Rais umelitekeleza kabisaa kwenye awamu ya tano umeunda wizara mbili
na hata tendo la leo linadhirisha kabisa jinsi ambavyo unazidi kuimarisha sekta
ya Nishati na Madini kwa hili tunakushukuru sana kwani linaonesha dhamira yako
ilivyo" alisema Ndugai
Mbali na
hilo Ndugai amesema kuwa katika miaka ya nyuma katika sekta ya madini na
nishati kama nchi tumeliwa sana hivyo anaamini kuwa katika Serikali ya awamu ya
tano chini ya Rais Magufuli na wateule wake jambo hilo halitaweza kuendelea
tena.
Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza mnamo Januari 30, 2018
Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment