Wizara
ya uchukuzi ya Afrika kusini imeanzisha uchunguzi kuhusu ajali ya treni
iliyotokea Alhamisi na kusababisha vifo vya watu 18 na wengine 239 kujeruhiwa.
Taarifa iliyotolewa na waziri wa uchukuzi wa Afrika
kusini Bw. Joe Maswanganyi, inasema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa ajali ya
treni kuacha reli ilisababishwa na lori lililojaribu kuvuka reli hiyo saa tatu
jana asubuhi wakati treni hiyo inapita, treni hiyo ya umeme iliwaka moto baada
ya kugonga lori na kusababisha vifo na majeruhi.
Waziri Maswanganyi alitembelea eneo la ajali na
kutoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga katika ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment