ASKOFU MNDOLWA ACHAGULIWA KUWA ASKOFU MKUU MTEULE WA ANGLIKANA


SINODI Maalum ya Kanisa la Anglikana Tanzania limemchagua Askofu wa dayosisi ya Tanga dokta MAIMBO MNDOLWA kuwa Askofu Mkuu wa saba wa Kanisa hilo.

Askofu MNDOLWA atakayeitumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano anamrithi askofu anayemaliza muda wake dokta JACOB CHIMELEDYA.

Akizungumza na waandishi wa habari feb 15 mjini Dodoma kuhusu uchaguzi huo Katibu Mkuu wa kanisa hilo Dokta MECKA OGUNDE amesema kikao cha uchaguzi kimefanyika kwa mujibu wa Katiba ya Kanisa hilo.

Kwa upande wake  Mwanasheria wa Kanisa hilo GEORGE MANDEPO amesema  Askofu huyo amepatikana kwa kupigiwa kura na maaskofu wa dayosisi 25 kati ya 28 zilizopo.

Askofu mkuu mteule MNDOLWA alipewa daraja la uaskofu na kuwekwa wakfu wa kuwa askofu wa Tanga septemba 4 mwaka 2012 ambapo mei 20 mwaka huu siku ya Pentekoste atasimikwa kuwa askofu mkuu katika ibada takatifu itakayofanyika katika Kanisa la Anglikana dayosisi ya Dodoma.



Share on Google Plus

About NYEMO FM RADIO

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment