Mkuu wa wilaya ya Chemba Simon Odunga akizungumza na maafisa wa jeshi la zimamoto katika zoezi la kuhamisha wananchi waliozingirwa na maji.
Wananchi wakihamisha mali zao kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji.
Wananchi wakihamisha mali zao kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji.
Wananchi wakihamisha mali zao kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji.
***********************************************************************
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Mwakisebe kata ya Kimaha wilayani
chemba mkoani Dodoma amefariki dunia, huku watu wengine zaidi ya 2000 wakiwa
hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kubomoka na nyingine kuzingirwa na
maji, kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha wilayani humo.
Wilaya ya Chemba ni miongoni mwa wilaya mpya zinazopatikana makao
makuu ya nchi Dodoma ambapo katika msimu wa mvua hizi za masika maeneo
mbalimbali ya mkoa wa Dodoma yamekuwa yakipata mvua nyingi zinazosababisha
mafuriko na adhari mbalimbali kujitokeza ikiwemo kuharibika kwa miundombinu ya
barabara.
Athari za mvua hizo zimejitokeza katika vijiji vya
Olboloti,Kaloleni na Mrijo Chini ambavyo ndivyo vinavyodaiwa kuwa ndio
vimeathiriwa zaidi na mafuriko hayo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kijiji cha
Olboloti Abdalah Suti amesema kuwa mvua iliyonyesha katika maeneo
yao ni kubwa na kwamba haijawahi kutokea tangu miaka ya 1960
Amiry Issa ni Mkuu wa zimamoto kituo cha Dodoma amesema kuwa
kikosi kinaendelea na shughuli za uokozi kuzunguka vijiji hivyo huku akiwataka
wananchi kutosogelea maeneo hatarishi
Akizungumzia hilo,Mkuu wa wilaya ya Chemba ambaye pia ni
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo, Simon Odunga amesema
kuwa eneo wanaloishi wananchi hao ni eneo hatarishi kwani wanazungukwa na
milima huku akiwataka wananchi waliojenga katika maeneo ya mabondeni kuhama
mara moja.
Chanzo: Full shangwe
0 comments:
Post a Comment