WABUNGE wa bunge la jumuiya ya Afrika mashariki
(EALA) wamesema wapo katika mchakato wa kuhakikisha wapata shilingi moja ya
afrika mashariki ambayo itasaidia wananchi wa jumuiya hiyo kufanya biashara
katika mazingira rafiki kwenye soko la pamoja.
Hayo yamebainishwa leo na
wabunge wa bunge hilo wakati wakizungumza na waandishi wa habari mjini hapa juu
ya ziara yao katika nchi zilizo katika ukanda wa kati ndani ya Jumuiya ya
afrika mashariki yenye nchi wanachama sita.
Nchi hizo wananchama ni
Tanzania, Kenya,Uganda,Burundi,Rwanda na sudani kusini.
Mbunge wa Bunge hilo Kutoka Tanzania
Maryam Ussi Yahya, amesema kuwa katika kuhakikisha wanachi wa nchi hizo
wanachama wa Jumuiya ya afrika mashariki (EALA) wananufaika na fursa zilizopo
kibiashara katika maeneo mbalimbali ipo haja ya kuwa na sarafu ya pamoja
itakayorahisisha biashara.
Amesema kuwa hivi sasa kumewepo
na changamoto ya sarafu kila nchi mwanachama kuwa na sarafu yake hali ambayo
inachangia kwa kiasi kikubwa kuwa kero kwa wananchi wanaotaka kufanya biashara
katika soko la pamoja.
Amesema sarafu hiyo ambayo
wanataka kuitengeneza sio jambo geni katika Jumuiya hiyo kwani tayari
ilishakuwepo katika miaka mingi ya nyuma ambayo ilikuwa ikitumika na nchi zote
wanachama wakati huo.
Naye mbunge wa Bunge hilo
kutoka Kenya Abdikadir Aden, amesema pia kazi ya jumuiya hiyo ni kuhakikisha
kuwa nchi wanachama zinakuwa na hali za utulivi kiasiasa ili kuwawezesha
wanachi wake kufurahia fursa zilizopo.
Katika ziara hiyo ambayo
wabunge hao wanaifanya nchini walianzia katika Taasisi ya kiswahi Zanzibar,
Bandari ya Dar es saalam pamoja na kujionea shughuli mbalimbali za kiutendaji
katika mizani ya kupimia mizigo kwenye magari ya Vigwaza.
Ziara hiyo ya wabunge hao
inalengo la kukagua na kuona changamoto zilizopo katika miundombinu namna
ambavyo inaweza kufanyiwa kazi ambapo pia watatembelea katika nchi za Burundi
na Rwanda.
0 comments:
Post a Comment