BAADHI ya wafanyabiashara wa
soko kuu la Majengo mkoani Dodoma wanaofanya biashara nje ya soko wameangua
vilio mbele ya Naibu waziri wa kazi,ajira na vijana Antony Mavunde kwa kile
walichodai kuwa wamekuwa wakichapwa viboko na baadhi ya kikosi cha mgambo wa
manispaa ya Dodoma.
Soko
kuu la Majengo mkoani Dodoma ni miongoni mwa masoko kongwe yaliyopo mkoani hapa
ambapo lilijengwa miaka ya 1996 lakini chakushangaza ni kuwepo kwa madai ya
wafanyabiashara hao kuchapwa viboko na mgambo wa manispaa.
Wakizungumza
kwa masikitiko wafanyabiashara hao wamesema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na
migambo ambao wamekuwa wakiwapiga na kuwadhalilisha huku wakitumia nafasi hiyo
kuiomba serikali kuwatafutia eneo mbadala la kufanyia biashara zao.
Akijibu
kero za wananchi hao diwani wa kata ya Majengo Msinta Mayaoyao amesema halmashauri
ya manispaa ya Dodoma wametenga fedha kwa ajili ya kujenga masoko ya kisasa ili
kuwasaidia wafanyabiashara kupata maeneo mazuri ya kufanyia biashara.
Akizungumzia
kuhusiana na kitendo cha wafanyabiashara kuchapwa fimbo na mgambo Naibu waziri
wa kazi,ajira na vijana Antony Mavunde ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Dodoma
amewataka mgambo hao kuacha vitendo hivyo kwani ni kinyume cha sheria.
Na Nazael Mkiramweni
0 comments:
Post a Comment