WAKULIMA WA KOROSHO WALIPWA MILIONI 8000





Deni la zaidi ya shilingi milioni 800 ambalo lilikuwa likidaiwa na wakulima wa Korosho kwa msimu wa 2016/2017 kwa vyama vya msingi (AMCOS) hatimaye limelipwa.

Mwenyekiti wa bodi ya chama kikuu cha ushirika cha Masasi, Mtwara Cooperative Union (MAMCU) Joseph Kidando amesema tayari kiasi hicho cha fedha kimeingizwa katika akaunti za vyama vya msingi kwaajili ya  kugawanywa kwa wakulima.

Aidha mwenyekiti huyo amesema wamelazimika kulipa deni hilo kutokana na wao kuwa walezi wa AMCOS na wakulima kwa ujumla na ametaja sababu za kuchelewesha kulipwa kwa fedha hizo ni upotevu wa fedha uliosababishwa na makosa ya viongozi wa AMCOS.

Kwa upande mwingine Kidando ameeleza kuwa sababu nyingine kubwa iliyosababisha upotevu wa fedha hizo ni kuingizwa kimakosa katika akaunti tofauti za vyama vya msingi, ambapo baadhi ya viongozi wasiowaaminifu waliamua kuzifanyia matumizi binafsi.

Chanzo: Mpekuzi
Share on Google Plus

About NYEMO FM RADIO

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment