Waasi wa Houthi warusha kombora mjini Riyadh

Jeshi la muungano linaloongozwa na Saudia linasema limezuia kombora lililorushwa kutoka Yemen kuelekezwa katika mji mkuu wa Riyadh.
Ripoti kutoka mjini humo zinasema kulisikika mlipuko mkubwa .
Mapema waasi wa Houthi walisema wamerusha kombora kulenga mojawapo ya maakazi ya ufalme wa Saudia huko mjini .
Muungano huo wa jeshi la Saudia umekuwa ukipigana na waasi hao wakiunga mkono serikali ya Yemeni katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosambaratisha kabisa nchi hiyo ya Yemen.
Waasi hao wa Kihouthi wanadaiwa kuungwa mkono na Iran na sasa Saudia inasema kombora hilo na lingine lililorushwa mwezi jana wanalichukulia kuwa uchokozi wa kivita kutoka Iran
Kombora hilo lililenga mkutano wa uongozi wa mamlaka ya Saudia katika eneo la al-Yamama mjini Riyadh ambapo mwanamfalme Mohammed bin Salman alitarajiwa kuzungumzia kuhusu bajeti ya kila mwaka ya ufalme huo.
Jumba hilo la kifalme ndio makao makuu ya afisi ya mfalme.
Dakika chache baadaye , kituo cha runinga cha al-Ikhbariya kiliripoti kwamba kombora hilo lilizuiliwa kusini mwa mji huoi mkuu.
Share on Google Plus

About NYEMO FM RADIO

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment