Polisi raia wa China waajiriwa Zambia

Polisi nchini Zambia imewateua raia 8 wa China kuwa polisi wa ziada.
Hatua hiyo imezua ghadhabu baada ya wakuu wa polisi mapema mwaka huu, kuwapiga marufuku polisi kutokana na kuoa raia wa kigeni kwa sababu za kiusalama.
Polis hao wa ziada walitajwa rasmi jana na mkuu wa polisi nchini Zambia na wanaaminika kuwa tayari wameanza kufanya kazi.
Dickson Jere, ambaye ni wakili, alisema kuwa uteuzi huo ulikiuka katiba ambayo inasema wazi kuwa, Mzambia yeyote aliye na uraia wa nchi mbili hawezi kujiunga na idara za usalama.
Msemaji wa polisi nchini Zambia Esther Mwata-Katongo, alitetea uteuzi huo wa polisi akisema kuwa kabla ya wao kuteuliwa walichunguzwa na watafanya kazi chini ya usimamizi wa polisi wa kawaida.

Share on Google Plus

About NYEMO FM RADIO

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment