WANAFUNZI waalimu
wa masomo ya Sayansi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ,wameombwa kutumia muda
wao wa ziada kujitolea kufundisha katika shule zilizopo karibu na chuo hicho
ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa waalimu wa sayansi .
Akizungumza na
waandishi wa habari mbele ya Kaimu Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Peter
Msoffe,mwanafunzi wa mwaka wa tatu kutoka Chuko Kikuu Kishiriki cha Dar es
Salam (DUCE) Emijidius Cornel amesema ambaye ndiye mwanzilishi wa kampeni ya
wanafunzi hao kujitolea amesema,wao kama wasomi wanapaswa kutumia
muda mwingi kujitolea kufundisha badala ya kutumia muda wao mwingi kuchati
kwenye Whatsap.
Cornel
amesema,hatua ya wanafunzi hao kujitolea,ni dhahiri itaweza kuongeza kiwango
cha ufaulu kwa mkoa wa Dodoma kwani wataziba pengo la upungufu wa walimu
hususani wa masomo ya sayansi katika baadhi ya shule za Dodoma mjini.
Rais wa Serikali
ya wanafunzi wa UDOM Francisco Nzalalila amesema,amelipokea wazo hilo na
atafanya utaratibu wa kuzungumza na wanafunzi wa masomo hayo chuo hapo ili
waanze mpango huo.
Amesema,wao kama
wanafunzi wasomi ,wanatamani kuwa sehemu ya kutatua changamoto za kielimu kwani
kwa hatua waliyofikia,uwezo wa kufanya hivyo wanao kwa muda ambao wanakuwa
hawana vipindi chuoni.
Kwa upande wake
Profesa Msoffe amesema,wazo hilo ni zuri kwani litawapa wanafunzi uzoefu wa
kufundisha darasani lakini pia watarudisha suala la uzalendo.
Hata hivyo
amesema kuwa tahadhari kubwa inatakiwa kuchukuliwa kwa wanafunzi hao waalimu
pindi watakapoenda kufundisha katika shule hizo.
Kutokana na
hayo Profesa Msoffe ametoa tahadhari katika mpango huo kwa kusema
wahusika watakiwa kufanya kazi kwa malengo ya kusaidia elimu nchini kupitia
wanavyuo hao
Halmashauri ya
manispaa ya dodoma inahitaji jumla ya waalimu 511 wa masomo ya sanaa lakini
waliopo ni waalimu 881 na hivyo kuwa na ziada ya waalimu 370 wa masomo hayo
huku mahitaji wa waalimu wa masomo ya sayansi ni 373 na walipo ni 258 ambapo
ina uhitaji wa waalimu wa masomo hayo 115.
0 comments:
Post a Comment