Mwakilishi wa Idara ya Jamii
kutoka halmashauri ya Kondoa Vijijini John Tesha amesema utekelezaji wa mradi
wa Afya Kinga mkoani Dodoma umesaidia kuongeza uelewa kwa wananchi kuzingatia
masuala ya usafi na hivyo Katika kujikinga na magonjwa mbalimbali ya mlipuko.
Ameeleza
hayo hapa mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kuhitimishwa kwa mkutano wa siku mbili wa Mkoa wa Uratibu wa Afya Kinga.
Amesema
kupitia utekelezaji wa mpango huo wananchi katika ngazi ya vijiji na vitongoji
imekuwa rahisi kwao kupata elimu ambayo imewawezesha kujua jinsi ya kujikinga
na magonjwa mbalimbali ikiwemo kufahamu namna ya kujenga vyoo bora
na kuvitumia,kutengeneza vifaa vya kunawa mikono watokapo chooni kwa njia
ya maji yanayotiririka na sabuni.
Naye
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Kondoa Dokta Ikaji Rashid amesema mradi huo
umekuwa na mafanikio makubwa sana kwa upande wa idara ya afya.
Kwa upande wake Afisa Afya Mkoa Carl Lyimo ameshukuru HPSS kupitia mradi wa Tuimarishe Afya kwa kutekeleza kwa vitendo kauli ya Kinga ni Bora Kuliko Tiba na kusema kwa muda mrefu eneo hilo halijafanyiwa kazi kwa kupewa kipaumbele na hata lilipopewa kipaumbele halijafanyika kwa utaratibu unaokubalika tofauti na hali ya sasa mkoani Dodoma.
Mkutano
huo umeratibiwa na Ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na
Mradi wa HPSS unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uswisi(SDC).
0 comments:
Post a Comment