Na Nazael Mkiramweni
Maafisa
elimu nchini wametakiwa kuwabainisha waalimu wanaofanya vitendo viovu
dhidi ya wanafunzi ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Akizungumza leo hapa mjini dodoma
wakati akifungua kikao cha kazi cha maafisa elimu wa mikoa na wilaya na makao
makuu ya wizara, WAZIRI wa nchi,ofisi ya rais,tawala za mikoa na serikali za
mitaa (TAMISEMI) Seleman Jaffo amesema
kuwa lengo la kikao hicho ni kujadili mipango,malengo na mikakati ya uboreshaji
elimu nchini.
Amesema walimu wana jukumu kubwa la
kusimamia nidhamu dhidi ya wanafunzi lakini kuna baadhi yao wamekuwa wakikiuka
maadili yao kwa kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi jambo
ambalo linakiuka maadili.
Kupitia kikao hicho Waziri Jaffo amemuagiza naibu katibu mkuu wa
tamisemi kuchunguza na kufanya maboresho ili mkoa wa Dodoma ambao ni makao makuu ya nchi uweze kufanya
vizuri katika sekta ya elimu.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa wizara
ya tamisemi Mhandisi Mussa Iyombe amewataka maafisa elimu
kujitathimini iwapo wanaiweza kazi hiyo .
Kufuatia maagizo hayo mwenyekiti wa
maafisa elimu wa mikoa na wilaya Mayasa Hashimu amesema kuwa watatekeleza
maelekezo na maagizo na kwamba kupitia kikao hicho wataweka maazimio ya
kiutendaji.
0 comments:
Post a Comment