Waziri wa nchi tawala za mikoa na serikali za mitaa, Tamisemi, Seleman Jaffo amekataa kuzindua mradi wa maji uliopo kijiji cha itiso kata ya itiso wilayani chamwino mkoani Dodoma.
Waziri Jaffo amekataa kuzindua mradi huo baada ya baadhi ya
wananchi wa kijiji hicho kuonyesha mabango ya kukataa kuzinduliwa kwa mradi huo
kwa kile walichodai kutoridhishwa na fedha zilizotumika.
Mhe.Jafo amefikia uamuzi huo hii leo asubuhi wakati alipofika
katika kijiji cha Itiso kwa lengo la kufungua mradi wa maji uliojengwa kwa
fedha za serikali lengo ikiwa ni kutatua Changamoto ya maji kwa wananchi wa kijiji hicho.
Katika hali ya kushangaza wananchi waliokuwa na mabango
walikataa kuzinduliwa kwa mradi huo kwa kile walichodai mradi kutoendana na
fedha zilizotumika.
Pamoja na kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na wananchi
hao,waziri Jafo amewashukru wataalamu waliojenga mradi huo kwa juhudi kubwa
walizofanya katika kutekeleza ujenzi wa huo.
0 comments:
Post a Comment