Dj Boss / Dj Rahim – Djs Bongo roho zenu zinawafanya mshindwe kuwa International Dj







Akiwa huko mbele yaani nchini Finland anafahamika kwa jina la Dj Rahm lakini kwa hapa Bongo Tanzania anakwenda kwa jina la Dj Boss
Jamaa huyu mkali wa kugusa mashine za kupigia mziki Dj Boss / Dj Rahim tangu amehamia ng’ambo ni miaka 24 iliyopita.

Hii leo ametembelea studio za Nyemo fm Radio na kukaribishwa katika kipindi cha Fleva Mixing ambacho hurushwa hewani kila siku za Jumamosi kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa sita kamili mchana.

Anasema kuna tofauti kubwa sana ya Dj’s wa Tanzania na mataifa mengine.

“ Tofauti kubwa sana iko katika Skills na kila mtu ambae ni International Dj lazima ni mtu ambae anashirikisha na kushirikishwa, lakini dj wa bongo wanaubinfsi sana kitu ambacho inakuwa ngumu kutoka,’’ Alisema Dj Rahm/ Dj Boss.

Anasema huko nje Madj wanashirikishana vitu vingi na wanajifunza kila siku hivyo amewashauri Djs wa Tanzania kuepuka kunyimana kazi na kwamba kila siku wajifunze vitu vipya.

Amesema Dj wa Tanzania bado hawajapewa vipaumbele na wamiliki wa Klabu kwani wengi hawaheshimiki wanabaki kuwa ni watu wa kusubiri kupiga mziki lakini kwa nchi nyingine wanajitegemea na wanamiliki vifaa vyao.

“ Huwezi kuwa Dj unaeheshika kama unasubiri kulipwa kwa mwezi hivyo Dj Tanzania waanze kujipanga kidogo kidogo na wamiliki vifaa vyao ili wale wenye klabu wawaite kwamba leo nahitaji kufanya kazi Dj huyu kwa makubaliano maalumu, “ Alisema

Aidha amezungumzia mziki wa Bongo ambapo amesema kwamba huko Finland mziki wa Bongo unakubalika na wasanii ambao wanaibeka Tanzania hasa ni Alikiba na Diamond.
 “ Basi wewe hutaamini sisi kila jumapili kuna hiyo Klabu inaitwa Afro Sunday, tumeianza mwaka jana mwezi tano lakini ndani ya miezi miwili tumekwenda mbali kwani ukiingia humo ndani mziki wa Afrika kwa Sehemu kubwa”.

“Kwa hiyo mziki wa Tanzania umekubalika sana Finland, wanajua alikiba ndo nani Dimond na wengine na hiyo si Finland tu kuna nchi kama Swedwen, Norway na Denmarka pia, “ Alisema Dj Boss.

Amewashauri Djs wa Tanzania kujituma na kufanya mazoezi kwa dhamira kwamba hata ukiamua kufanya mazoezi yasipungue saa 20 bila kupumzika ili kujijengea uwezo zaidi.

Share on Google Plus

About NYEMO FM RADIO

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment