*KWA UFUPI TAARIFA YA KUTOKEA MAAFURIKO KWENYE KATA YA MRIJO WILAYANI CHEMBA, MKOANI DODOMA, JAN 9,2018 (Nyumba 1000 zazingirwa na Maji)*






Mvua kubwa zilizonyesha usiku wa kuamkia Januari 9, 2018 Wilayani Chemba Kata ya Mrijo  mkoani Dodoma, zimesababisha athari kubwa kwenye vijiji vitatu vya kata hiyo 

Vijiji vya Kata hiyo vilivyoathiriwa ni Mrijo Chini,  Kaloleni na Olboroti ambapo taarifa ya awali ya tathimini ya Wilaya ya Chemba inaonesha Takribani nyumba 1000 zimezingirwa na maji

Taarifa hiyo ya Tathimini pia inaonesha takribani Nyumba 70 zimedondoka kwa mchanganuo ufuatao: Elboroti-39, Kaloleni-22, Mrijo Chini-9

Wenyeji wa eneo hilo wanasema Hali kama hiyo iliwahi kujitokeza miaka ya 1968 na kuwa sehemu hiyo ni eneo la mkondo wa maji na kipindi hiko maji yakituama yalikuwa yakitumika kunywesha mifugo, Lkn badae Wananchi wakagaiwa viwanja na kujenga

Taarifa ya Tathimini ya awali  pia inaonesha Wananchi walioathiriwa na mafuriko hayo wamepoteza  mifugo na vifaa vya majumbani.

Uongozi wa Wilaya ya Chemba umelazimika kuzifunga shule mbili kwa Kuwa zimezingirwa na maji na hivyo siyo sehemu salama kwa Wanafunzi, shule ya msingi kaloleni na shule ya Sekondari Mrijo

Hakuna mtu aliyepoteza maisha kufuatia mafuriko hayo, Tathimini ya Kina inaendelea kufanyika kubaini athari zaidi na mahitaji halisi ya Wananchi  wahanga ili kuweza kuwasaidia.

Wananchi wameopolewa kutoka eneo la mabondeni ambapo maji yamezingira nyumba za Wananchi, na Wananchi wachache waliobakia Kazi ya kuwatoa mabondeni kwenye maji kuwapeleka eneo la makazi yaliyopo maeneo ya muinuko inaendelea Hadi kufikia usiku wa Januari 9.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma limewekwa Kambi eneo Hilo kuhakikisha Wananchi wote wanatolewa eneo lenye maji na kupelekwa eneo salama kwa Usalama

Serikali imeandaa makazi eneo la shule kwa ajili ya Wananchi wale watakaokosa hifadhi kwa ndugu jamaa na marafiki

Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Nkamia kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba Dkt. Mashimba wametoa mahindi Gunia 50 kwa ajili ya kusaidia Wananchi hao wahanga.

Serikali ya Wilaya ya Chemba imetenga Maghala mawili kwa ajili ya kuhifadhia baadhi ya Mali za Wananchi zilizofanikiwa kuopolewa kwenye eneo lililoathirika kwa maji, na tayari wameweka ulinzi

Kufuatia Hali hiyo,  MKuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Stano Mahenge akiambatana na Wajumbe WA Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma wamefika eneo la tukio kuwajulia Hali Wananchi, kuwapa pole na kuona Hali halisi ya athari zilizotokea

Mbunge wa Chemba Mhe. Nkamia amemwomba MKuu wa Mkoa kuhakikisha Serikali inachukua hatua ili Wananchi WALIOJENGA  na kuishi mabondeni WAHAME na kunusuru Maisha Yao na kusisitiza Maisha ya Wananchi yasifanyiwe Siasa,  amewataka Wananchi WA Kata nzima ya Mrijo na vijiji vyake kuweka itikadi za Siasa pembeni na kusaidiana kwenye janga hili kwani mafuriko hayachagui itikadi za siasa

Mkuu wa Wilaya ya Chemba Simon Odunga amemwelezea MKuu wa Mkoa Kuwa kwa Sasa Changamoto nyingine ni kukatika   kwa mawasiliano ya Barabara inayounganisha kata ya Mrijo Chemba na Mji wa Kiteto

Mkuu WA Mkoa Dkt. Mahenge ameambatana na Wataalamu WA TANROADS ili kufanya kazi ya kurudisha miundombinu ya Barabara

Serikali ya Wilaya kwa Kushirikiana na  Mkoa wanazungumza na Wadau mbalimbali na Ofisi ya Waziri MKuu ili kupata msaada wa mahitaji mbalimbali na kuyapleka kwa Wananchi kwa haraka

*RC Dkt. Mahenge amesisitiza Wananchi wa eneo la Mrijo Kuwa kitu kimoja kushikamana na kusaidiana kwenye janga hili kwa Wananchi walio kwenye makazi salama kusitiri wenzao wahanga

*Ili kuhakikisha Usalama na kunusuru maisha ya Wananchi  kwenye  waliokuwa wanaishi mabondeni, RC Dom Dkt. Mahenge amewapiga marufuku Wananchi hao  wasirudi tena kwenye makazi Yao kwa Kuwa eneo Hilo siyo salama tena kwa Kuwa mvua zinaendelea kunyesha.

#RC Dkt Mahenge amewaagiza wataalamu wa Wilaya ya Chemba kwenda kupima eneo lililozingirwa na maji ili kubaini Wananchi wasiotakiwa kurudi tena kwenye eneo Hilo la makazi. 

#RC Dkt Mahenge amemwagiza MKuu wa Wilaya Mkurugenzi na Wataalamu wa Halmashauri ya Chemba kuwapimia Wananchi viwanja vipya vya makazi kwenye eneo lililoinuka na salama kwa makazi ili Wananchi wajenge makazi mapya

#Wananchi wahanga kwenye eneo Hilo wameridhia maelekezo ya Serikali na kuomba zoezi la kuwapimia lifanyike kwa uharaka ili wajenge makazi mapya na salama

#RC Dkt Mahenge: Uharibifu wa Mazingira kama ukataji miti hovyo ndio umeleta mabadiliko haya ya Tabia ya NChi yenye athari Kama hizi za mvua na mafuriko,  Ameagiza Kampeni ya Upandaji miti eneo Hilo na miche ya miti ipo ya kutosha

#RC Dkt Mahenge: Nimeagiza Timu ya Wataalamu wa Afya wafike haraka eneo la tukio na kuchukua hatua muhimu kuhakikisha wanazuia magonjwa yote ya mlipuko yanayoweza kutokea, na athari zingine kiafya

#RC Dkt Mahenge: Naagiza Wakuu wa Wilaya Wote,  Wakurugenzi wa Halmashauri Wote,   Makatibu Tarafa Wote na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa  muhakikishe Wananchi wote wanaoishi mabondeni  wanahama mara moja kama tahadhari  ya mvua  zinazoendelea kunyesha hapa Mkoani Dodoma.

*Imetolewa na:*
Ofisi ya MKuu wa Mkoa Dodoma
Januari 9, 2018

Share on Google Plus

About NYEMO FM RADIO

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment