Baada ya kukosa udhamini wa SportPesa AFC Leopards na Gor Mahia huenda zikajiondoa michuano ya CAF


Huenda klabu za AFC Leopards na Gor Mahia zikajiondoa katika michuano ya CAF endapo zitakosa udhamini kutoka sportpesa ambao wapo katika mvutano na kutokana na nyongeza ya kodi kwa kampuni ya bahati nasibu.
Leopards maarufu Ingwe wamepangiwa kucheza na FOSA Juniors ya Madacascar katika mechi ya kombe la CAF, lakini wanahitaji kiasi cha Sh30 milioni kugharamia mikondo yote miwili, pesa ambazo mwenyekiti wao, Dan Mule amesema haziwezi kupatikana bila usaidizi wa SportPesa ambao ndio wadhamini wao wakuu. Serikali imeingia vitani na SportPesa kutokana na uamuzi wake wa kuzitaka kampuni zote za kamari nchini zitozwe asilimia 35.
Mahasimu wao wakuu, Gor Mahia ambao watawakilisha taifa katika michuano ya klabu bingwa Afrika, pia wanakabiliwa na shida hiyo kwa vile SportPesa ndio wadhamini wao. K'Ogalo wamepangiwa kucheza na Leones Vegetarianos ya Equatorial Guinea katika raundi ya kwanza.


Share on Google Plus

About NYEMO FM RADIO

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment