Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Wadau wa Habari Dodoma
Mwanahabari Mkongwe Edna Ndejembi akizungumza katika mkutano wa wadau mkoani Dodoma.
Mlezi
wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma(CPC) Daniel Msangya
akichangia katika mkutano wa wadau wa habari wa mkoa huo.
Mwanahabari Idd Maalim akichangia kwenye mkutano wa wadau wa habari Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino akizungumza katika mkutano wa wadau wa habari Dodoma.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
WADAU
wa habari mkoa wa Dodoma wameshauriwa kutumia wanahabari katika
kuchochea mipango na shughuli mbalimbali za maendeleo kwenye ngazi zote
za utawala ili kuhabarisha umma.
Kauli
hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Athuman Masasi
katika mkutano uliowakutanisha wadau wa habari mkoa wa Dodoma ambao
ulilenga kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu uhusino baina yao na
wanahabari na upatikanaji habari zinahusu maendeleo ya mkoa huo.
Mkutano
huo uliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Dodoma(CPC) kwa
ufadhili wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari nchini(UTPC) ambao
hufanyika kila mwaka.
Akichangia
majadiliano kwenye mkutano huo, Masasi alisema tasnia ya habari ni
muhimu kwa ustawi wa Mkoa huo na Taifa kwa ujumla na kuwahakikishia
wanahabari kuwa halmashauri za mkoa wa Dodoma kwa sasa zina mipango na
shughuli nyingi za maendeleo hivyo zinahitaji wanahabari kufikisha
taarifa hizo kwa wananchi.
Aidha
aliwaomba wanahabari kuwasiliana na mamlaka za serikali hasa pale
wanapopata taarifa za tatizo lolote ili kujua juhudi za serikali za
kupambana nalo.
Naye,
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Dodoma(CPC), Habel
Chidawali aliwataka waandishi kuondokana na uandishi wa mazoea ili
kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano.
Aidha
aliwaomba wadau katika mkoa wa Dodoma kuvitumia vyombo vya habari
katika kutangaza fursa zinazopatikana katika maeneo yao kwa kuwa vina
uwezo wa kufikia kundi kubwa la wananchi.
Naye, Mwandishi mkongwe nchini, Edna Ndejembi alisema kuwa ili Mkoa wa Dodoma uweze kufikia maendeleo yake hauna budi kuvitumia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kwani kwa kufanya hivyo utatoa fursa kubwa kwa wadau kujitokeza na kuwekeza mkoani hapa.
Alisema
mkoa wa Dodoma una fursa nyingi kwenye Nyanja mbalimbali ikiwemo kilimo
cha zabibu ambazo zinahitaji kutangazwa ili kupata wawekezaji na
kuwezesha mji huo kukua hasa ikizingatiwa tayari umepewa hadhi ya kuwa
Jiji.
Pamoja
na hayo, Mlezi wa CPC Daniel msangya alisisitiza waandishi kujiendeleza
kielimu na kujisoma vitabu na sheria mbalimbali ili kuweza kufanya kazi
zao kwa ufanisi.
0 comments:
Post a Comment