Imebainika kuwa asilimia 48 ya wanaoishi na
Virusi Vya Ukimwi (VVU) hawajapima kujua afya zao ambapo asilimia 52 pekee
walio na virusi hivyo ndio wanaodaiwa kupima kubaini hali zao.
Imeelezwa watu 81,000 Tanzania
wanaambukizwa maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa mwaka na watu 200
huambukizwa maambukizi hayo kwa siku,ambapo kati yake 50 ni vijana.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi
mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) ,Leonard Maboko wakati
akifungua mkutano wa mpango mkakati wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo kwa kushirikiana
na waandishi wa habari Mjini Kibaha mkoani Pwani.
Amesema ukimwi bado ni tishio na ni
ajali kama zilivyo ajali nyingine ambayo haionekani lakini ni ajali mbaya
kutokana na kusababisha maambukizi mapya kila siku kwa watu 200.
Amesema Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania
inatarajia kuanza kampeni za kitaifa
kuhamasisha wanaume kupima afya zao ,ili kujenga tabia ya kujitokeza kupima
kwani ni asilimia 45 pekee ya kundi hilo walioaminika kuwa na VVU ndio
waliopima kujua hali zao na kwamba kampeni hiyo itakuwa ya miezi sita na
itakuwa endelevu hadi hapo watakapohakikisha wanatokomeza ama kupunguza
maambukizi .
0 comments:
Post a Comment