Wizara ya ulinzi ya Russia imesema ndege moja ya
mzigo ya jeshi la Russia aina ya An-26 ilianguka jana kwenye kituo cha jeshi la
anga cha Khmeimim nchini Syria, na kusababisha vifo vya watu wote 32 waliokuwa
kwenye ndege hiyo, wakiwemo wafanyakazi 6 na abiria 26.
Kwa mujibu wa wizara hiyo, ndege hiyo ilianguka
mita 500 kutoka barabara ya ndege wakati ikijaribu kutua kwenye kituo hicho.
Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa wakati ajali inapotokea ndege hiyo
haikushambuliwa, na chanzo cha ajali hiyo kinaweza kuwa hitilafu za kiufundi.
0 comments:
Post a Comment