Mkuu wa wilaya
ya mpwapwa jabir shekimweri amemsimamisha kazi mweka hazina wa
halmashauri hiyo na watendaji wanne kupisha uchunguzi kutokana na ubadhirifu wa
fedha za mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.
Hatua hiyo imechukuliwa na Mkuu wa wilaya hiyo wakati akipokea ripoti ya tume aliyoiunda kutokana na ubadhirifu
wa fedha za mapato ya halmashauri zaidi ya shilingi milioni 500.
Awali
akisoma ripoti ya tume ya ya uchunguzi wa sakata hilo mwenyekiti wa tume hiyo
edwin kitullo alibainisha tume ilivyofanya kazi yake kufuatia hadidu kumi za
rejea na kutoa mapendekezo ya tume.
Mwenyekiti
wa halmashauri hiyo donald ngwenzi ambaye ni diwani wa kata ya masa akawashukia
madiwani kutosimamia ukusanyaji wa mapato vizuri katika kata zao jambo ambalo
limepelekea ubadhirifu.
Baada ya
tume kusoma taarifa na kumkabidhi mkuu wa wilaya ya mpwapwa alichukua maamuzi ya
kumsimamisha kazi mweka hazina wa halmashauri hiyo Michael Amanzi na watendaji
4 wa kata na kuwatupa ndani kwa saa 48,kwa amri ya mkuu wa wilaya hadi hapo
uchunguzi utakapokamilika.
0 comments:
Post a Comment