Kutokuwepo kwa miundombinu ya uhakika na ukosefu wa pedi za kujisitiri kwa watoto wa kike pindi wananapokuwa katika hedhi kumeonekana kuchangia watoto kushindwa kuhudhuria masomo katika shule ya Sekondari Mwanzi iliyopo wilayani Manyoni.
Katika
kutatua changamoto hiyo shirika lisilo la kiserikali CAMFED kwa kushirikiana na
wizara ya elimu na mafunzo hapa nchini imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa
watoto 60 wa kike waishio katika mazingira magumu.
Akikabidhi
msaada huo Mbunge wa jimbo la Manyoni Mshariki Daniel Mtuka amesema gharama ya
vifaa vyote ni milioni 13 na laki 8 hivyo amewataka wazazi kutozitumia baiskeli
na vifaa vingine kwa manufaa yao bali vitumike kama ilivyo lengwa ili
viwanufaishe wanafunzi hao.
Vilevile
mbunge huyo amewasisitizia watoto hao wa kike kusoma kwa bidii na kukaa mbali na
mambo mengine ya anasa ili kutimiza ndoto zao Kimaisha.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Manyoni Magembe Machibula amewasisitiza wazazi wa watoto hao kushirikiana na watoto wao kutunza vifaa walivyopokea.
Naye mkuu wa shule ya Sekondari Mwanzi Janeth Lubas amelishukuru shirika hilo kwa msaada huo na kwamba utasaidia kupunguza utoro shuleni hapo.
Esteria Nathan mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo kwa niaba ya wanafunzi wenzake amesema kupitia msaada huo jamii itegemee matunda mazuri kutoka kwa wanafunzi wa shule hiyo.
0 comments:
Post a Comment