Jukwaa la wanawake Chamwino ( JUWACHA ) laiomba Serikali kuongeza bajeti katika sekta ya afya, elimu na Kilimo ili kukidhi mahitaji ya jamii.

Jukwaa la wanawake Chamwino ( JUWACHA ) linalofanya shughuli zake chini ya Shirika la Action Aid wameiomba Serikali kuongeza bajeti katika sekta ya afya, elimu na Kilimo ili kukidhi mahitaji ya jamii. Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa na Jukwaa la Wanawake Chamwino chini ya shirika la Action Aid iliyotolewa March 29 mwaka huu wilayani Chamwino. Akiwasilisha matokeo ya utafiti uliofanywa na jukwaa hilo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Chamwino ( JUWACHA ) Janeth Nyamayasi, amesema Vituo vingi vya afya vimeonekana kuwa na Changamoto kadhaa zikiwemo ukosefu wa vifaa kama vitanda vya kujifungulia, wodi za wanawake na madawa ya kutotosheleza. Amesema ongezeko la wanafunzi na uhaba wa walimu mashuleni limekuwa ni tatizo kubwa huku akitolea mifano shule ya msingi Chita ambayo ina wanafunzi 814 na walimu 6, Iringa Mvumi yenye wanafunzi 948 na walimu 8 pamoja na shule ya msingi Mloda yenye wanafunzi 1100 na walimu 10. Mmoja wa wanajukwaa hilo Baton Mdoe amesema Maafisa kilimo ni wachache ukilinganisha na idadi ya watu na kwamba hata vitendea kazi kwa maafisa hao bado ni Changamoto inayokwamisha sekta hiyo. Kwa upande wao Afisa Elimu Wilaya ya Chamwino, Daud Mwamalasi,Andrew Kaymgoya kutoka ofisi ya Mganga Mkuu Wilaya na Aithan Chaula ambae ni Afisa Kilimo wilaya ya Chamwino wamekiri kuwepo kwa hali hiyo. Kutoka na hali hiyo ni dhahiri Upatikanaji wa huduma za jamii katika Sekta ya afya, elimu na Kilimo haiendani na mikakati madhubuti ya kutoa huduma kwa Jamii.
Share on Google Plus

About NYEMO FM RADIO

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment