Halmashauri ya wilaya ya Bahi yapokea billion 25.7





Halmashauri ya wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma imepokea jumla ya shilingi billion 25.7 ikiwa ni ongezeko la asilimia 8 zaidi ya bajeti iliyoidhinishwa katika mwaka wa fedha 2016/2017.

Bajeti iliyoidhinishwa katika halmashauri hiyo  ni shilingi billion 23.9 ambapo hadi kufikia mwezi June walikuwa wamekwisha pokea kiasi cha shilingi billion 25.7 sawa na asilimia 108 ya bajeti.

Aidha katika mwaka huo wa fedha halmashauri hiyo imetumia kiasi cha shilingi bilioni 21.2 ikiwa ni sawa na asilimia 82.5 ya fedha zilizotolewa.

Taarifa hiyo imetolewa wilayani humo na kaimu afisa mipango ambaye pia ni mchumi wa wilaya hiyo NRIGI URASA katika kikao maalum cha baraza la wafanyakazi kwa ajili ya kupitisha mpango na bajeti ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019.

Urasa ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha julai 2016 hadi juni 2017, kuwa ni ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mchito, ambao umekamilika na kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma ya maji kutoka asilimia 38.50 hadi kufikia asilimia 38.90.

Aidha katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 halmashauri hiyo iliidhinishiwa bajeti ya shilingi bilioni 30.6 ambapo hadi kufikia disemba 2017 jumla ya shilingi bilioni 10.1 sawa na asilimia 33 ya bajeti iliyoidhinishwa kilikuwa kimeshatolewa.

Halmashauri hiyo imeomba maombi maalum ya shilingi bilioni 3.6 kwa ajili ya kusaidia kujenga mtandao wa maji makao makuu ya wilaya, ujenzi wa jengo la utawala hospitlai ya wilaya ya Bahi, madeni ya watumishi na ununuzi wa magari matatu kwa ajili ya elimu ya msinigi, sekondari na mkaguzi wa ndani.

Share on Google Plus

About NYEMO FM RADIO

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment