HALMASHAURI YA USHETU YAPIGA MARUFUKU UVUNAJI HOLELA WA MITI KWENYE MAENEO YA TAASISI ZA UMMA
Halmashauri ya ushetu wilayani Kahama Mkoani Shinyanga,imepiga
marufuku uvunaji holela wa miti kwenye maeneo yote ya taasisi za
umma zikiwemo shule ,zahanati na vituo vya afya bila kibali kutoka
mamlaka husika.
Agizo hilo limetolewa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo
Michael Matomola kwenye mkutano wa hadhara wakati akizungumza na
wakazi wa kijiji cha Ifunde baada ya kubaini kuwepo kwa uvunaji holela
wa miti katika shule ya msingi Ifunde.
Amesema serikali kwa sasa inaendesha kampeni ya upandaji wa miti nchi
nzima hivyo ni kosa la jinai kwa mtumishi wa umma ama mwananchi kukata
miti iliyopandwa kwenye maeneo ya umma bila kufuata taratibu za
kisheria.
Sanjari na hayo,Matomola amewataka wananchi katika halmashauri hiyo
kujenga vyoo bora katika nyumba zao ili kujiepusha magonjwa ya mlipuko
ikiwa ni pamoja na kipindupindu.
0 comments:
Post a Comment