Ushirikishwaji wa
watumishi wa kada mbalimbali kwenye masuala ya Afya Kinga umeelezwa kusaidia
kuondokana na changamoto ya uhaba wa wataalam wa masuala hayo.
Mwakilishi kutoka Idara ya Lishe na ustawi wa Jamii Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)GERALD KIDOGO ameeleza hayo
katika mkutano wa kimkoa wa siku
mbili kwa ajili ya Uratibu wa Afya Kinga mkoani Dodoma.
Kidogo amesema pamoja na serikali kuweka sera na miongozo ambayo
inatekelezwa na Ofisi hiyo changamoto iliyopo ni ya watumishi wa kada hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala
Halmashauri ya wilaya ya Kondoa KILAJA ARKANUS amesema kwa muundo wa
halmashauri kuna idara 13 katika kutafuta ufanisi kwenye shughuli za usafi au
afya kinga ambapo idara zimehusishwa.
Mkutano
huo umeratibiwa na Ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa wa Dodoma kwa
kushirikiana na Mradi wa HPSS wa Tuimarishe Afya unaofadhiliwa na Shirika la
Maendeleo la Uswisi(SDC).
0 comments:
Post a Comment