Idara ya Uhamiaji
imewatangaza maofisa 18 wa ngazi tofauti kutohusika ama kutambua huduma yoyote
itakayotolewa nao kwa sababu si wafanyakazi tena.
Hatua
hiyo imetokana na idara hiyo hivi karibuni kupokea malalamiko mengi kupitia
kampuni na taasisi mbalimbali kuwa kuna watu wanapita kwenye ofisi
wakijitambulisha kuwa maofisa kutoka uhamiaji.
Msemaji
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanda, jana alisema kutokana na hali
hiyo, wameamua kuwatangaza watu hao ambao baadhi walisimamishwa kwa makosa ya
rushwa na utovu wa nidhamu.
Mtanda
alisema idara ya Uhamiaji iliwasimamisha kazi watu hao mwaka 2016/17 na kwamba
wengine waliacha kazi wenyewe.
Alisema wameamua
kufanya hivyo ili chochote kitakachojitokeza dhidi yao, idara haitahusika.
“Tumeamua
kuwatangaza kwa sababu hivi karibuni tumepokea malalamiko mengi kupitia kampuni
na taasisi mbalimbali kuwa kuna watu wanapita kwenye ofisi hizo
wakijitambulisha kuwa maofisa kutoka uhamiaji.
“Hawa
tuliowatangaza leo (jana) kuwa sio wafanyakazi tena wa Idara ya Uhamiaji lengo
ni ili jambo lolote likitokea huko nje dhidi yao itambulike si watumishi wetu
tena,” alisema.
Mtanda
alisema orodha hiyo ambayo imeambatanishwa na picha za watu hao ni kwa lengo la
umma kuwatambua kuwa si wafanyakazi wa idara hiyo tena.
Katika
tangazo lililotolewa juzi na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, idara hiyo
haitahusika au kutambua huduma yoyote itakayotolewa na watajwa kwenye picha.
Watu hao
ni Thobias Lyewe, Julieth Mrema, Nina Muga, Loveness Wilson, Wilbard Ompapson,
Salama Dilunga, Philbert Chaula, Mkombozi Chodri na Alfred Mrema.
Wengine
ni Imaculata Mwakatika, Ramadhani Ally, Ritha Maganga, Jovin Mkuchu, Veronika
Max, Angel Mwambwiga, Peter Bally, Elizabeth
Kibinga na Lucy Munyanga.
0 comments:
Post a Comment