Siku moja baada ya wanafunzi kumi na saba kuuawa kwa kupigwa risasi huko Marekani, chama cha Democrats kimewashutumu Rais Donald Trump na Spika wa bunge la nchi hiyo Paul Ryan kwa kukataa kuruhusu mjadala wa sheria ya kumiliki silaha.
Wakati waMarekani wakiwa bado wanaendelea kuomboleza kifo cha wanafunzi 17 waliuawa kwa kupigwa risasi kumekuwa na wito wa nchi hiyo kubadili sheria ya kumiliki silaha.
Akizungumzia mauaji hayo Rais wa Marekani Donald Trump awali katika hotuba yake amesema usalama katika shule utakuwa ni moja ya mambo yatakayopewa kipau mbele. Hata hivyo alishindwa kulishauri bunge la nchi hiyo lipitie upya sheria ya kumiliki silaha.
"Utawala wetu unafanya kazi kwa karibu na mamlaka za eneo la mji kuchunguza tukio la kupigwa risasi na kupata taarifa zote iwezekanavyo. Tumejitolea kufanya kazi na jimbo pamoja na viongozi wa eneo hilo kusaidia kulinda usalama wa shule na kukabiliana na masuala magumu yanayotokana na matatizo ya afya ya akili." Alisema Trump
Mwanafunzi aliyefanya mauaji hayo, alifukuzwa shule kwa utovu wa nidhamu katika shule moja huko katika jimbo la Florida.
Akihutubia katika tukio hilo Baba wa mwanafunzi wa mika 14 aliyeuawa kwenye tukio hilo Fred Guttenberg amesema familia yake imeumia kutoka na kifo mtoto wao.
''..Hii haiwezekani. binti yangu , mtoto wangu mwenye umri wa miaka 14. na kwenu mnaojua binti yangu Jamie, alikuwa ni maisha katika burudani. Alikuwa anatutia nguvu tukio nyumbani. Alisema kwa masikitiko
Chanzo: BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment