SERIKALI
imetangaza msimamo wake kwa watumishi ambao walibainika kuwa na vyeti feki na
wale wasiokuwa na vyeti vya kidato cha nne kuwa hawana madai yoyote ya kuidai
serikali baada ya Rais John Magufuli kutangaza kufanyika kwa uhakiki kwa
watumishi wa umma.
Hayo
yameelezwa na Mkurugenzi wa idara ya uendelezaji sera, Mathias
Kabundugulu,wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi cha kujadili masuala ya
utawala na rasilimali watu kwa mamlaka za serikali za mitaa, wizara na mikoa.
Amesema
watumishi ambao wamebainika na kuondoka wenyewe, wamefutwa kwenye orodha ya
watumishi wa umma na hawana madai wanayodai serikalini huku amesema pamoja na
zoezi hilo kukamilika kwa muda ambao umepangwa, wapo baadhi ya maafisa utumishi
wameendelea kuwafumbia macho watu wasiokuwa na vyeti vya kidato cha nne.
Naye
katibu mkuu wa wizara ya Tamisemi, Mhandisi Mussa Iyombe, amesema kumekuwepo na
changamoto mbalimbali zinazofanywa na maafisa wa utumishi katika halmashauri mbalimbali
nchini.
Selemani
Jafo ni Waziri wa nchi, ofisi ya rais, tawala za mikoa na serikali za mitaa,
Tamisemi, , amewataka makatibu wakuu wa wizara yake na wale wa ofisi ya rais
utumishi, kuangalia upya miongozo na sheria ambazo zimekuwa kandamizi kwa
watumishi wa umma.
0 comments:
Post a Comment