Mcheza tennis mwenye umri wa miaka 36, Roger Federer amekuwa
mchezaji wa kwanza mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kutokea kwa zaidi ya miaka
mitano katika historia ya mchezo huo na kuvunja rekodi ya Andre Agassi
aliyestaafu akiwa na umri wa miaka 33 mwaka 2003.
Federer ameandika historia hiyo baada
ya hapo jana kushinda mchezo wake dhidi ya Robin Haase katika michuano ya dunia
ya tennis ya ABN Amro inayo endelea huko Rotterdam.
Mchezaji
huyo anayeshika nafasi ya pili katika viwango vya ubora duniani amesema kuwa
anahitaji kuwa nafasi ya kwanza ambayo inashikiliwa na Rafael Nadal “Kushika
nafasi ya kwanza nimoja ya lengo langu,”amesema Federa ambaye mchezo ujao
anatarajia kukutana na Andreas Seppi aliyemshinda Muitalia Daniil Medvedev
kwa seti 7-6(4) 4-6 6-3.
0 comments:
Post a Comment