Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma atangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake ya Urais


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake ya Urais kwa manufaa ya Chama chake cha ANC na Wananchi wa Afrika Kusini.

Zuma ametangaza hadharani kujiuzulu kupitia vyombo mbalimbali vya habari katika matangazo yaliyokuwa yanarushwa LIVE. Uamuzi wa Zuma umekuja kutokana na msukumo uliokuwa unatolewa na Chama chake pamoja Bunge la nchi hiyo.

Mapema jana februari 14, 2018 Ofisi ya rais nchini Afrika kusini iliviambia vyombo vya habari kusubiri taarifa rasmi ya mkutano na waandishi habari pamoja na rais Jacob Zuma, huku kukiwa na matarajio kwamba anakaribia kujiuzulu kuwa mkuu wa nchi hiyo.
Taarifa ya ofisi ya rais ilikuja baada ya taarifa za vyombo vya habari kuwa Zuma atalihutubia taifa kujibu amri ya chama tawala cha ANC kwamba analazimika kujiuzulu kuwa rais wa taifa hilo.
Wakati huo huo polisi Afrika kusini iliwakamata watu watatu kutoka katika familia tajiri nchini humo baada ya kuvamia makaazi ya familia hiyo inayoshukiwa kutumia mahusiano yao na rais Jacob Zuma kushawishi uteuzi wa nyadhifa za baraza la mawaziri na kupata kandarasi za taifa.
Polisi kutoka kitengo cha upelelezi waliingia katika eneo la makaazi ya familia ya Gupta jana katika kitongoji cha Saxonwold, eneo linaloishi watu wa kipato cha juu mjini Johannesburg.
Share on Google Plus

About NYEMO FM RADIO

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment