WINGA wa kimataifa wa Tanzania,
Simon Happygod Msuva jana ameendeleza moto wa mabao baada ya kuifungia timu
yake, Difaa Hassan El Jadida katika sare ya 3-3 na wenyeji, Chabab Atlas
Khénifra Uwanja wa Manispaa ya Khenifra kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco,
maarufu kama Botola Pro.
Msuva alifunga bao lake dakika ya 42, wakati mabao mengine ya Jadida
yalifungwa na watokea benchi Anouar Jayid dakika ya 82 na Adnane El Ouardy
dakika ya 90 na ushei, wakati ya wenyeji yalifungwa na I. Elbas dakika ya nane,
H. Merchand dakika ya 11 na K Pacero dakika ya 57.
Sare
hiyo inaosogeza Difaa Hassan El Jadida nafasi ya nne kwenye msimamo wa Botola,
ikifikisha pointi 25 baada ya kucheza mechi 16, ikiwa inazidiwa pointi sita na
vinara, Raja Casablanca.
Ikumbwe, mwishoni mwa wiki, Msuva alifunga mabao matatu peke yake katika
ushindi wa 10-0 dhidi ya Benfica ya Guinea Bissau kwenye mchezo wa kwanza wa
Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El
Jadida, Mazghan nchini.
0 comments:
Post a Comment