Mbunge
wa jimbo la Dodoma mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na
Ajira, Mhe. Antony Mavunde amesema
hapati usingizi wa kutosha kwani mda mwingi huutumia kutafuta njia ya kutatua
Changamoto ya maji na Umeme jimboni kwake.
Hayo aliyasema
leo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na Nyemo fm radio iliyopo mjini Dodoma kupitia
kipindi cha Dunia Yetu ambacho hurushwa hewani kila siku za Jumamosi kuanzia
saa moja kamili asubuhi hadi saa tatu kamili asubuhi.
Alisema
pamoja na mafanikio makubwa aliyopata katika kutekeleza ahadi zake alizozitoa
wakati wa Kampeini za uchaguzi mwaka 2015 kwenye sekta ya elimu, afya na
Miundombinu bado kuna Changamoto kubwa katika kutatua changamoto ya maji na umeme.
“Kwa
kweli kwa kiwango kikubwa sana najivunia kuziishishi ahadi zangu katika
kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Dodoma ,” alisema.
Mavunde
ameongeza kuwa yeye binafsi anafarijika kwa kuzigusa ahadi zake kwa asilimia
kubwa na kwamba furaha itakamilika zaidi
mara baada ya kukamilisha yote aliyoyahaidi katika jimbo la Dodoma.
Alisema
anaamini kwa nafasi yake ya Ubunge bado anazo nguvu na ataendelea kutafuta
fursa za kuwaletea maendeleo wananchi wake ili kuondokana na adha ya siku
nyingi ambayo wananchi wamekuwa wakiilalamikia ya kushindwa kupata maendeleo.
“ Sina
makwazo lakini kuna jambo linanisumbua ambalo ni kero kubwa ya maji na umeme
katika maeneo ya pembezoni naamini nikikamilisha hilo hata mimi nitapata
usingizi walau wa masaa manne katika masaa nane ambayo mwanadamu anapaswa
kulala,” alisema Antony Mavunde.
0 comments:
Post a Comment