Mchezaji soka Tanzania Himid Mao
‘Ninja’, leo anatarajiwa kuondoka Dar es Salaam kwenda mjini Cape Town, Afrika
Kusini kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa goti la mguu wake kulia
linalomsumbua.
Ninja ambaye amekosa takribani mechi nne zilizopita za Azam FC baada ya
kupewa mapumziko maalum kupisha matibabu ya tatizo hilo, pia ni Nahodha wa
kikosi cha wachezaji wanaocheza nyumbani cha timu ya taifa, ‘Taifa Stars’.
Kiungo huyo wa ulinzi anayeweza kucheza kama beki pia, ni mchezaji tegemeo wa klabu na timu ya taifa.

Daktari Mkuu wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa, amesema kuwa Nahodha huyo
Msaidizi wa Stars atafanyiwa uchunguzi huo katika Hospitali ya Vincent Pallotti
mjini humo ili kujua undani wa tatizo lake huku akidai ataanza kuchukuliwa
vipimo na Dk. Nickolas Ijumaa hii.
“Himid
amekuwa akicheza na maumivu makali katika goti la kulia na tulimzuia kucheza
mechi baada ya mechi mbili zilizoita baada ya kuona yale maumivu yanaendelea na
tulifanya vipimo vya M.R.I ambavyo vilionyesha kuna hitilafu kwenye goti lake
na alipata matibabu katika Hospitali ya Moi (Muhimbili).
“Lakini baada ya kupata matibabu takribani wiki moja tuliamua ni busara zaidi kumpeleka katika Hospitali ya Vincent Pallotti nchini Afrika Kusini kwenda kuangaliwa zaidi ukiangalia Himid bado ana majukumu ya klabu na makubwa ya timu ya Taifa vilevile kama nahodha,” alisema.

Katika hatua nyingine, Mwankemwa alithibitisha kuwa mshambuliaji wa timu
hiyo, Wazir Junior, anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo wa mguu katika kitengo
cha Moi, Hospitali ya Muhimbili mjini Dar es Salaam baada ya donge la damu
kuvilia chini ya mguu.
“Wazir (Junior) alikuwa na tatizo kwenye kifundo cha mguu na tumemfanyia vipimo vyote vya M.R.I, X-Ray, alikuwa akitibiwa Moi sasa hivi taratibu zinafanyika matibabu ya zaidi yatakuwa katika Hospitali ya Moi, ambayo atafanyiwa upasuaji mdogo baada ya kujulikana kuwa chini ya mguu kuna bonge la damu kwa hiyo tunatarajia ndani ya siku mbili hizi Junior kufanyiwa upasuaji huo,” alisema.

Akizungumzia matibabu ya beki Daniel Amoah, anayesumbuliwa na maumivu ya
goti, alisema kuwa wanatarajia kufanya taratibu za kumfanyia kipimo cha M.R.I
na kuangalia tatizo linalomkabili ndani ya goti hilo.
“Mtakumbuka siku ya mechi yetu na Stand United alianguka kandokando ya kiwanja na kujiumiza lakini tulikuwa tukimuuguza na kumpatia madawa akapata nafuu akacheza mechi ya Simba, lakini baada ya mechi ya Simba yale maumivu yamejirudia tena na sasa tunafanya taratibu za kumfanyia kipimo cha M.R.I…na baada ya kupata majibu ya M.R,I tutawafahamisheni zaidi ni jinsi gani matibabu yake yatakuaje,” alisema.

0 comments:
Post a Comment