Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoani Dododma Gilles Muroto amewaagiza viongozi wa dini
kuhakikisha maeneo yao wanayofanyia ibada kunakuwa na ulinzi wakutosha ili kuzuia
matukio ya kiuhalifu.
Hayo yamesemwa Februari 14, 2018 na kamanda wa polisi mkoani
humo, Kamishna msaidizi Mwandamizi wa polisi, Gilles Muroto.
Kamanda
Muroto amesema kuwa kutokana na kukua kwa utandawazi kumekuwa rahisi kwa sasa
watu kutumia nafasi hiyo kupotosha umma huku wakijinadi kuwa ni viongozi wa
dini.
Muroto
amesema viongozi wa dini watakaobainika kufanya vitendo hivyo au vya aina
yoyote ile ya udhalilishaji jeshi la polisi halitawavumilia.
Aidha amewaonya viongozi wa dini ambao wanatabia ya kufanya
vitendo vilivyo kinyume na mafundisho ya dini huku likiwaomba wananchi
wawafichue viongozi hao ambao wenye tabia hizo.
0 comments:
Post a Comment