China yahimiza utekelezaji wa mkakati wa kustawisha vijiji


Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China leo imetoa waraka wa kwanza wa mwaka 2018 unaoelekeza utekelezaji wa mkakati wa kustawisha maeneo ya vijijini.

Waraka huo umesema, kutekeleza mkakati wa kustawisha maeneo ya vijijini ni matakwa ya lazima ya kutatua mgongano kati ya mahitaji ya wananchi yanayoongezeka siku hadi siku ya kutafuta maisha bora na maendeleo yasiyo na uwiano, pia ni matakwa ya lazima ya kutimiza utajiri wa wananchi wote.
Kwa mujibu wa waraka huo, pamoja na mambo mengine, China itainua ubora wa maendeleo ya kilimo, kuhimiza maendeleo vijijini yasiyo na uchafuzi, kustawisha utamaduni wa vijijini, kujenga utaratibu mpya wa usimamizi wa maeneo ya vijijini, na kuinua kiwango cha uhakikisho wa maisha ya wakazi wa maeneo ya vijijini.
Share on Google Plus

About NYEMO FM RADIO

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment