BAADA YA MAJIMAJI KUPIGWA 4G NA YANGA JANA LEO MWADUI WANATUA DIMBANI DHIDI YA SIMBA ..



Mwadui FC leo inawakaribisha Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.

Mwadui wataingia katika mchezo wa leo wakiwa na kumbukumbu ya kuchapwa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza, Septemba 17, mwaka jana Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Na kipigo hicho walipewa wakati Simba SC bado inafundishwa na kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog, kabla ya kumfukuza na kumleta Mfaransa Pierre Lechantre.
Simba SC inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa dhamira ya kushinda na kuendelea kujiweka vizuri kwenye uongozi wa Ligi Kuu katika harakati za kutwaa ubingwa wake wa kwanza baada ya miaka mitano.

Kwa sasa, Simba SC wanaongoza Ligi Kuu wakiwa na pointi 41, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 37, wakati Azam FC wanashika nafasi ya tatu kwa pointi zao 34.
Ligi Kuu itaendelea kesho, Lipuli FC wakiwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Samora mjini Iringa, wakati keshokutwa kutakuwa na mechi mbili, Njombe Mji FC wakiwakaribisha Maji Maji ya Songea Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe na Kagera Sugar wakiwa wenyeji wa Singida United Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Mechi moja tu itachezwa Jumapili, Mbeya City wakiikaribisha Stand United Uwanja wa Sokoine, wakati Jumatatu kutakuwa na mechi mbili pia, Tanzania Prisons na Mwadui FC Uwanja wa Sokoine na Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Share on Google Plus

About NYEMO FM RADIO

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment