Sehemu ya shehena ya samaki wachanga waliokaushwa kwa chumvi aina ya Sangara
kilo 65600 waliokamatwa katika kisiwa cha Lubili wilayani Muleba, wakiwa
wamehifadhiwa katika ghala kwenye ofisi ya Uvuvi jijini Bukoba. Samaki hao
walikaatwa kufuatia raia mwema kutoa taarifa kwa Waziri Luhaga Mpina hivi karibuni.

Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson
Mpina amekamata kilo 65600 za samaki wachanga aina ya Sangara waliokaushwa kwa
chumvi wenye thamani ya shilingi milioni mia tatu katika Kisiwa cha Lubili
wilayani Muleba kwenye Mkoa wa Kagera baada ya wamiliki wa samaki hao kukimbia.
Akizungumza leo na
Waandishi wa Habari katika Ofisi ya Kitengo cha Doria na Udhibiti wa
Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera, Mpina amesema tukio la kukamatwa
kwa samaki hao lilifanikiwa baada ya yeye kupata taarifa kutoka kwa raia
mwema ambapo aliagiza mamlaka za Wilaya ya Muleba kufuatilia kwa karibu
hatimaye kuwakuta samaki hao wakiwa wameanikwa chini katika kisiwa hicho.
Waziri Mpina
alisema Sheria ya Uvuvi namba 22 ya Mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka
2009 kifungu cha 90(1) inataka samaki wanaovuliwa waandaliwe katika mazingira
yanayokidhi vigezo vya usalama kwa mlaji na kwamba ni kosa kisheria
kuwavua au kuchakata samaki aina ya Sangara walio chini ya sentimeta 50 kwa
kuwa ni wachanga na sentimita 25kwa Samaki aina ya Sato. Pia sentimita 85 kwa
Sangara kwa kuwa ni wazazi wanaotakiwa kundelea kuzaa.
Aidha Waziri aliongeza
kwamba Sheria hiyo imetoa mamlaka kwa watendaji wa Serikali kutaifisha
mali zote zilitumika katika uvuvi haramu kupitia kifungu cha 37(a) (ii)
na (iii) pamoja na Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu
namba 29 ya mwaka 1994.
Waziri Mpina
ameagiza watendaji kufuata taratibu zote za kisheria ili samaki hao
wauzwe kwa njia ya mnada na mapato hayo yaingie Serikalini mara moja.Aidha
aliwaonya wafanyabiashara na wavuvi kuachana na uvuvi haramu kwa kuwa ni
kuhujumu raslimali za taifa ambazo zingetumika kwa kizazi cha sasa
na baadaye.
“Mfanyabiashara yoyote wa
samaki na mazao yake anayetaka kufilisika na kutafuta matatizo katika
maisha yake aendelee na biashara ya uvuvi haramu”alisisitiza Mpina
maisha yake aendelee na biashara ya uvuvi haramu”alisisitiza Mpina
Kufuatia tukio hili,
Waziri Mpina amewapa wiki mbili wafanyabiashara na wasafirishaji wote wa
samaki na mazao yake waliopewa
leseni ya ya kufanya biashara hiyo kwa mwaka 2018 kuleta cheti cha uthibitisho cha ulipaji kodi ambapo amesema kama watashindwa
kufanya hivyo hawataruhusiwa kufanya biashara hiyo.
leseni ya ya kufanya biashara hiyo kwa mwaka 2018 kuleta cheti cha uthibitisho cha ulipaji kodi ambapo amesema kama watashindwa
kufanya hivyo hawataruhusiwa kufanya biashara hiyo.
Alisema kuanzia sasa
wafanyabiashara wote wote wataruhusiwa kupata leseni hiyo baada ya
kuwasilisha cheti cha uthibitisho wa ulipaji kodi, cheti cha usajili wa kampuni
na mahesabu ya kibiashara yaliyohakikiwa ili kuepuka utaratibu wa sasa
ambao unatoa mwanya kwa mawakala wa ndani na nje ya nchi kujiingiza katika
biashara hiyo kinyemela na kuikosesha Serikali mapato kwa kukwepa
kulipa kodi
mbalimbali.
mbalimbali.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu alisema Serikali
itahakikisha kwamba uvuvi haramu unakuwa historia katika Mkoa wa Kagera na
kuwataka wananchi kuwafichua wavuvi haramu ili vyombo vya Serikali
viwakamate na kuwafikisha katika mikondo ya sheria.
Alisema sekta ya
uvuvi inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuinua hali ya uchumi
kwenye mkoa wake na taifa kwa ujumla
kama wadau wote watashiriki kikamilifu katika vita dhidi ya uvuvi haramu ambapo alisema jumla ya wananchi 26,272
wameajiriwa kutokana na shughuli za uvuvi katika mkoa huo.
kama wadau wote watashiriki kikamilifu katika vita dhidi ya uvuvi haramu ambapo alisema jumla ya wananchi 26,272
wameajiriwa kutokana na shughuli za uvuvi katika mkoa huo.
Alisema mkoa utaendelea
na kupambana na uvuvi haramu ambapo kwa mwaka 2016/17 jumla ya doria 65
zilifanyika na kuwezesha kukamatwa kwa makokoro ya Sangara 422, nyavu ndogo za
dagaa 57,nyavu za timba 3,231, nyavu za makila 14,141, ndoano 711, katuli
16,mitumbwi 133 samaki wachanga kilo 5,621 na watuhumiwa 86.
16,mitumbwi 133 samaki wachanga kilo 5,621 na watuhumiwa 86.
Hata hivyo Mkuu
huyo alisema katika kuongeza uzalishaji wa samaki jumla ya mabwawa 584
yamechimbwa kwa mwaka 2016/2017 kutoka mabwawa 181 mwaka 2005/2006 sawa na
ongezeko la mabwawa 403.
Kwa upande mwingine Mkuu
wa Mkoa alisema hivi karibuni Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara
ilikamata gari lenye namba za uasajili T 614 CLQ aina ya Mitsubishi Canter
likiwa limepakia samaki kilo 2,000 aina ya Sangara na kilo 530 wa aina ya Sato
kwenye mpaka wa Murusagamba wilayani Ngara.
Alisema Afisa wa
Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera
bwana Ayoub Ngoma
na dereva wa gari hilo Ayoub Sanga walishikiliwa na polisi kwa hatua za kisheria kwa tuhuma za kushiriki
katika utoroshaji wa samaki wenye kilo 2530 kwenda nchini Burundi zenye thamani ya shilingi 20,850,000/= ambapo Ngoma
ameshasimamishwa kazi kupisha uchunguzi.

Pia Mshauri wa Uvuvi wa
Mkuu wa Mkoa, Efrazi Mkama na maafisa Uvuvi wa Halmashauri ya Muleba
Wilfred Tibendelana na Maengo Nchimani na Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Bukoba vijijini Renus Ruhuzi wanaendelea kuripoti katika kituo cha polisi
Bukoba kwa mahojiano ya kisheria juu ya utoroshwaji wa samaki hao.
Bukoba kwa mahojiano ya kisheria juu ya utoroshwaji wa samaki hao.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara
ya Maendeleo ya Uvuvi, Mwanaidi Mlolwa alisema Serikali ina mkono
mrefu na kwamba hakuna mtu
atakayebaki salama iwapo atajihusisha na uvuvi haramu.
atakayebaki salama iwapo atajihusisha na uvuvi haramu.
Aidha alisema maafisa
uvuvi wanawajibu wa kuhifadhi na kutunza takwimu mbalimbali za sekta ya uvuvi
ili kutoa picha halisi ya jinsi
sekta inavyochangia katika uchumi wa nchi kwa ujumla.
sekta inavyochangia katika uchumi wa nchi kwa ujumla.
“Kimsingi sekta ya uvuvi
ina mchango mkubwa katika uchumi wa
nchi yetu lakini tatizo kubwa ni ukosefu wa takwimu sahihi
nchi yetu lakini tatizo kubwa ni ukosefu wa takwimu sahihi
0 comments:
Post a Comment