Mamlaka ya Mapato Tanzania imetoa wito kwa wamiliki
wote wa vyombo vya moto kwamba kuanzia sasa yoyote atakaepoteza kadi ya gari
atatakiwa kutoa tangazo kwenye Gazeti.
Akizungumza na Nyemo fm mapema leo, Afisa
mwandamizi huduma na elimu kwa mlipa kodi Barnabas John Masika
alisema zoezi hilo linaanza mara moja.
Alisema
yeyote atakaepoteza kadi atatakiwa kutoa tangazo la kupotelewa kadi hiyo kwenye
gazeti pamoja na taarifa ya upotevu kutoka kituo cha Polisi na nakala za
taarifa hizo zipelekwe kwenye ofisi za TRA ili kupata nakala nyingine ya kadi.
0 comments:
Post a Comment