Mwenyekiti
wa Bodi ya Parole Tanzania, Augustino Mrema amelitaka Jeshi la Polisi na
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kumchukulia hatua aliyezusha taarifa za
kifo chake Januari 9 mwaka huu.
Mrema ambaye ni Mwenyekiti wa TLP Taifa ameyasema
hayo mapema leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nje ya Kituo cha
Polisi jijini Dar es Salaam alipokwenda kuripoti tukio hilo.
Amesema, aliyezusha taarifa hiyo alifahamu kwamba
Lowassa amekwenda Ikulu kuonana na Rais Dkt Magufuli, hivyo akazusha uongo ili
watu wasiwe makini kuhusu kilichojadiliwa Ikulu.
Mrema amesema wapinzani wa Rais ndio walizusha
taarifa hizo za uongo na kuzua taharuki kwa sababu yeye ni mtu maarufu na
wanajua kwamba kwa kufanya hivyo wangesababisha watu kutofautilia
kilichozungumza Ikulu.
Baada ya kusema hayo, Mrema ameweka wazi kwamba
anataka kulipwa fidia ya TZS 20 bilioni kutokana na kuzushiwa kifo na kwamba
fedha hiyo haitapungua hata shilingi mia.
Chanzo. Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment