Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amemtolea uvivu mkuu wa wilaya ya Nyasa, Isabella Chilumba na mkurugenzi wa
halmashauri hiyo, Dk Oscar Mbyuzi, ambao wamekuwa wakivurugana, akisema tofauti
zao zinaathiri watendaji walio chini yao na kuumiza wananchi.
Taarifa
iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu inasema kuwa Majaliwa alisema hayo
alipokuwa katika ziara yake Wilaya ya Nyasa.
Waziri
Mkuu alisema katika ziara zote za mikoani, amekuwa akipata malalamiko mengi
kwenye halmashauri na mabaraza ya madiwani, lakini amekuta hali si shwari
Wilaya ya Nyasa kwa kuwa kuna migogoro midogo kwenye uongozi wa juu.
“Tatizo
ni dogo huku juu, bado mnavurugana mkuu wa wilaya na mkurugenzi. Ninyi ni
viongozi wa juu, acheni kuvurugana, fanyeni kazi. Mkigombana wanaoumia ni
wananchi,” alisema.
“Mkuu wa
wilaya anaweza kuingia kwenye kikao chochote cha halmashauri na kudai apewe
taarifa, mpeni. Yeye siyo mjumbe wa kikao hicho, lakini anayo mamlaka ya
kushiriki.
“Mkurugenzi
ni mtendaji mkuu, tumekukabidhi watumishi uwaongoze. Tumekukabidhi fedha kwa
ajili ya maendeleo ya wilaya hii. Mtu akizitamani, mwambie hizi fedha zina
maelekezo rasmi, hazipaswi kwenda kokote.”
Aliwataka
madiwani wasijenge tabia ya kuongeza siku za vikao kwa makusudi ili tu wapate
posho za ziada.
“Msitengeneze
siku za ziada na kumpa presha Mkurugenzi. Kama kikao ni cha siku moja, basi
kiishe. Siyo kulaza ajenda ili mmalizie kesho yake. Mkurugenzi akiwanyima
fedha, msianze kugombana naye kwa sababu yeye hana fedha za kumgawia mtu,”
alisisitiza.
0 comments:
Post a Comment